Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa Zesco wa Zambia
Timu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa beki wa Zesco ya nchini Zambia, Mkongomani Marcel Kalonda ambaye anatumia guu la kushoto na ni mkali katika kukaba katika ile staili ya mtu na mtu ‘man to man’.
Uwezo wake huo unaweza kuwa kikwazo kwa viungo wasumbufu kwenye ligi kama Clatous Chama, Luis Miquissone pamoja na mastaika kama John Bocco na Prince Dube.
Kalonda, 23, mkataba wake na Zesco unatarajiwa kumalizika Desemba 31, mwaka huu hivyo huenda akaja kuchukua nafasi ya Mghana Lamine Moro ambaye tayari Yanga imetangaza kuachana naye Alhamisi.
Yanga imepanga kukiboresha kikosi chao ili kifanye vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kocha Nasreddine Nabi ndiye anayetajwa kupendekeza jina la beki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba, kupunguza na kuanzisha mashambulizi kwenye goli la wapinzani.
“Katika kikao cha Jumatano jioni kilichowakutanisha Kamati ya Mashindano ya Yanga na kocha Nabi, jina la Kalonda lilitajwa katika mipango yetu ya usajili.
“Jina hilo lilikuja baada ya kocha na kamati kukubaliana kwa pamoja kuachana na Moro.
“Hivyo yapo baadhi ya majina yaliyokuwa yamewekwa mezani yaliyokuwa yanapitiwa na Kalonda lilikuwepo pamoja na beki raia wa Benin, Partene Counou. Hivyo mmoja kati ya hao huenda akawa mbadala wa Moro,” alisema mtoa taarifa huyo.
Akizungumzia usajili huo, Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla alisema: “Kikubwa Wanayanga wawe watulivu, tumepanga kufanya
usajili bora utakaofanikisha malengo yetu katika msimu ujao, tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa wachezaji wetu na mara baada ya kukamilika tutaweka wazi kila kitu.”
from Udaku Special https://ift.tt/3rSgjBG
via IFTTT
Comments
Post a Comment