Mwakinyo "Ngumi za Kulipwa si za Kugombania Beberu Wala Gari"


Ninaposema hakuna mtu wa kupigananae Tanzania, haimaanishi mimi ni bora kuliko watu wote au hakuna mtu atakaeweza kunipiga. Huu ni mchezo ngumi hazina mwenyewe.

Mimi nina heshimu nilipo kwa sababu najua nilipotoka, leo kuna ma-boxer wengi sana lakini ukimzungumzia Mwakinyo ni pekeyake kwa sababu rekodi yangu haifanani na ya mtu yeyote.

Kwa hiyo, apatikane kwanza mtu mwenye rekodi kama ya Mwakinyo, ili nitakapopigananae mbali ya kupata pesa tu lakini ikitokea nimepoteza sishuki kwenye viwango vya ubora kwa sababu nimepigwa na bingwa.

Mfano, bondia nitakayepinanae [Julius Indongo] sina wasiwasi hata akinipiga sishuki kwenye viwango vya ubora kwa sababu ameshacheza na watu wakubwa zaidi yangu lakini nikimpiga haitashtua, watu watanisifu na kwenye ubora haitanipandisha sana kwa sababu tayari nipo juu.

Mtu akishafikia kwenye ubora nilipo mimi tunaweza kukaa kuzungumza nalipwaje ili tupigane sio kuandika kwenye mitandao kwamba kuna beberu linagombaniwa. Ngumi za kulipwa hazipo hivyo.

Mimi nina uongozi, hata unapomtaka mwanamke kwa ajili ya kuoa kuna taratibu zake sio kuandika kwenye mitandao mimi nataka kumuoa fulani.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3kFsiPR
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI