Mwana FA Afunguka Kuhusu Afya yake Usiku Huu na Jinsi Ajali ilivyotokea


"Tulikua wawili mimi na Dereva wangu tulitoka Muheza tukapita Msoga Rais Mstaafu alikua amefiwa na Mtoto wa Kaka yake tukaenda mazikoni pale, tukawa tunatoka tunaelekea Dodoma hii sehemu inaitwa Kingolwira kuna malori mengi yanaelekea Dar kuna Mtu akawa ana overtake"

"Alikuja upande wetu na yuko spidi sana tunamuona kabisa hivi, spidi yake ilikua kubwa kusema kweli nafikiri kati ya 140 au 160 hivi na tunamuona kabisa anakuja na hatukuwa na namna yoyote ya kumkwepa, tunashukuru tu Mungu tumetoka salama mimi nina maumivu kidogo kifuani na mkono wa kushoto lakini napata huduma hapa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kama unavyoona Mh. Mkuu wa Mkoa na Mh. Mkuu wa Wilaya wapo hapa kuhakikisha kila kitu kinakua sawa" ——— Mbunge wa Muheza Tanga Mh. Hamis Mwinjuma @MwanaFA.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/2WCaXi8
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI