Simba yaandika Rekodi Al Ahly...Kumfunga na Kuwauzia Mchazaji Kwa Bei Kubwa




ACHANA na rekodi za kuwafunga kila mara wanapokanyaga kwenye Uwanja wa Mkapa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imeandika rekodi nyingine dhidi ya Al Ahly ya Misri. Luis Jose waliyemuuza kwa Ahly kwa zaidi ya Sh2 bilioni amekuwa raia wa kwanza wa Msumbiji kucheza kwenye klabu hiyo kwa mujibu wa historia.

Hakuna mchezaji yeyote raia wa nchi hiyo aliyewahi kuchezea klabu hiyo kabla kwa mujibu wa rekodi zilizoko kwenye makumbusho ya Ahly jijini Cairo.

Lakini kwenye Ligi ya Misri anakuwa ni wa pili baada ya mkongwe wa ENPPI, Mano ambaye naye si mchezo.

Simba ilimuuza Luis baada ya Kocha Pitso Mosimane kushinikiza kwamba anamtaka baada ya kuona makali yake kwenye Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Habari za uhakika zinadai kwamba Wekundu hao walishindwa kuvumilia kuacha fedha za Ahly kwani ni nyingi ambazo wanaweza kufanyia mambo mengine ikiwamo kuvuta mashine mpya.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/38vgt9a
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI