Baada ya Marioo Kunusurika Kipigo Arusha, Meneja Wake wa Zamani Afunguka



Fundi wa muziki wa Bongo Flava, Marioo ambaye alidai chini ya milioni 20 hafanyi show kibongo bongo, inaripotiwa kuwa weekend iliyopita alikuwa na show Arusha ambayo alilipwa kiasi cha sh. Milioni 15 lakini Show ikaingia mdudu baada ya Marioo kuchelewa kufika kwa wakati na raia kuanza kufanya vurugu ikiwemo kuharibu Mali na kutaka kutembeza kichapo kwa Marioo na timu yake.

Hasa kupitia U-HEARD ya XXL na @soudybrown ,meneja wa zamani wa Marioo na C.E.O wa Daddy Entertainment Co. , @d_fighter1 ametoa neno kwa msanii huyo kwanza akimpa pole maana ni changamoto ya kazi lakini pia amedai kufanya tena kazi na Marioo sidhani kama itakuwa rahisi kwasasa, kwanza anahisi watu alionao hivi sasa ndio watu aliowahitaji na kuona watamfikisha sehemu lakini pia kuachana na Msanii huyo ni kutokana na kauli yake aliyodai anahitaji kupoteza baadhi ya vitu kwenye maisha yake ili apate vikubwa zaidi na baada ya hapo likaja suala la Marioo kutotaka kuendelea na D Fighter kama meneja wake tena.

Kwasasa D Fighter ni meneja wa msanii wa kike anayekuja kwa kasi kwenye ramani ya muziki wa Bongo Flava, @saraphina__tz

Machalii wa R hawapakagi rangi upepo😁 ukizingua unachezea.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3CVECmo
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI