Hasheem Thabeet Anacheza Basket Hapa Tanzania? Aisaidia Timu ya Savio Kutwaa Ubingwa RBA

 


Timu ya mpira wa Kikapu ya Savio wametwaa ubingwa wa Ligi ya mpira wa kikapu Dar es salaam RBA baada ya kushinda mchezo wa tatu (3) wa fainali kwenye mfululizo wa michezo mitano (5) ya fainali baada ya kuibuka na ushindi wa alama 99 kwa 83 dhidi ya ABC kwenye mchezo wanne (Game 4).

Mchezaji nyota wa Savio Hasheem Thabeet alifunga jumla ya alama 52 pekee yake kati ya alama 99 zilizowapa ushindi hapo jana, lakini pia alimaliza na rebound 15 pasi za kufunga (Assists) 3 na alifanya Blocks 6.

Katika mfululizo wa michezo hiyo ya fainali Savio walishinda mchezo wa kwanza (Game 1) kwa alama 82 kwa 73, ABC wakashinda mchezo wa pili (Game2) kwa 82-79 na mchezo wa 3 ( Game 3) walishinda Savio kwa alama 83-64, kabla ya kushinda tena jana na kuongoza kwa 3-1 kwenye michezo minne (4 ) na sasa rasmi Savio ndio mabingwa wa RBA



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/2Wrmt09
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI