Mtazamo Wangu Kujiuzulu Kwa Mo Dewji Simba "Mwepesi Kubebwa na Presha za Matokeo"
Kuhusu neno KUJIUZULU ni la kawaida duniani kote, mpirani, siasa na hata kwenye mapenzi! Hakuna mgeni kwenye hili
Ramon Calderon aliwahi kujiuzulu Urais wa Real Madrid na kupisha uchaguzi Mkuu uliomleta Perez kwa awamu ya pili na ikumbukwe hata Perez aliwahi pia kujiuzulu
Perez aliwahi kusema kitu kuhusu watu KUJIUZULU, alisema kuna muda mambo hayaendi kisa wewe, kuna muda unajiona nje ya mfumo na kuhitaji mwingine aongoze na kuna muda masherti kadhaa
Well! MO DEWJI wa Simba kajiuzulu Uenyekiti wa klabu ya Simba na majukumu anayo Try Again! Naomba hapa niseme kitu kuhusu MASHERTI
Moja wapo ya matakwa ya FCC ni kuwa huwezi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na bado ukawa Mwekezaji kwenye timu, ni sawa na kusema kesi ya Nyani umpe Ngedere, hapa walitaka kuondoka CONFLICTS OF INTERESTS
Kujiuzulu kwa MO ni dalili za wazi hivi sasa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa Simba unaenda kutimia rasmi kwakuwa hata FCC walisema mchakato upo mwishoni kukamilika, pongezi kwa MO
Sababu nyingine ya MO kujiuzulu ni kutokana na ratiba yake! Ni ngumu Mwenyekiti kuwa nje ya nchi zaidi ya miezi mitatu hata kama teknolojia imepiga hatua ila Bodi ni shughuli za kila siku
Mambo mengi yalikuwa hayaendi kutokana na kukosekana kwake, hivyo kujiuzulu kwake kunaleta Mwenyekiti ambae atapatikana kwa muda wote na kujihusisha na shughuli zote
FARHAN unasemaje kuhusu MO kujiuzulu? To me ni uamuzi mzuri kwa maslahi ya klabu as long as anasalia kuwa Investor basi hakuna shida, hii pia itasaidia kuondoa presha, MO personally alikuwa mwepesi kubebwa na presha ya matokeo haswa kutweet😄 (utani tu)
Hawa wakina Salim wanazijua presha, wanajua kuishi nazo kwakuwa wamezizoea sana
By @jr_farhanjr
#MOROGORO
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3iiI2rp
via IFTTT
Comments
Post a Comment