Mvua yasitisha kwa muda Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake
Jaji Mustapha Siyani anayesikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu amesitisha kwa muda kusikiliza ushahidi wa shahidi watatu upande wa utetezi wa shauri dogo katika kesi ya msingi ya Uhujumu Uchumi kutokana na kukosekana kwa usikivu mzuri unaosababishwa na mvua inayonyesha.
Leo mapema shahidi wa tatu upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu alianza kutoa ushahidi wake katika Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3um2vk0
via IFTTT
Comments
Post a Comment