MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI
Mpenzi mwandani mahabubu Naanza kwa kukuomba samahani Kuandika kwa lugha hii legevu Nilijaribu lakini sikuweza Kuyasarifu maneno matamu Kwa lugha muafaka ya kimapenzi Mara nyingine ninaahidi Kutakalamu kwa lugha inayofaa Bidii nitafanya Kuyaelewa machungu na matamu yanguKwa lugha tukufu isiyo yangu Badala ya hiki kishairi duni, Nitakwandikia poem Nitajitahidi mpenzi Maneno kuyaelewa Si kwa jicho la kwangu kijijni Bali kwa mboni na urazini wa kule kulikotukuka Nitayatongoza machozi yangu Kububujika kwa vokali na konsonanti za kimombo Makali ya moyo wangu kulipuka kwa Kireno, Kitaliani au Kituruki Badala ya huu msamiati nilokujazia hapa, Nitakuwa na vocabulary Mpenzi nitakusifu Kwa majina ya mimea, wanyama na ndege Wasiopatikana kwetuNitakutungia koja Nilirembe kwa vito na maua ya nchi za baridi Au mimea ya jangwaniNisamehe kwa sasa mpenzi Naikumbuka tu lugha yangu Ilonitoa tumboni mwa mama Ninajua mpenzi Ni vigumu kwangu kujie
Comments
Post a Comment