Ndugai Awakosoa Mawaziri, Ataka Bunge Kutolaumiwa Kwa Kila Jambo





Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuna changamoto ya baadhi ya mawaziri na mwanasheria mkuu wa Serikali (AG) hali inayosababisha baadhi ya sheria kurejeshwa tena bungeni kurekebishwa muda mfupi baada ya kupitishwa.
Ndugai alitoa kauli hiyo jana Jumamosi Oktoba 30, 2021 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya mawaziri na naibu mawaziri yaliyoandaliwa na taasisi ya uongozi.

"Wakati mwingine unaona hii aah..., lakini waziri anang’ang’ana kwa kawaida wabunge watasema sawa ipite ukienda huko hata miaka miwili haishi unarudi na amendment (marekebisho),” amesema akisisitiza kuwa ndio maana kila mkutano wa Bunge kuna muswada wa marekebisho ya sheria.

Amesema kama marekebishi yangekuwa yanakuja mara moja moja ni sawa kwa sababu yangekuwa ni marekebisho yaliyopitwa na muda lakini si kama ilivyo sasa.

Amesema kwa sababu ya muda hawezi kutaja baadhi ya sheria zilizoliaibisha Bunge na kwamba inapotokea hivyo hawatajwi mawaziri wala Serikali bali inakuwa mzigo wa Bunge na wabunge.


“Ndio mwisho wanasema hili Bunge la Ndugai ni takataka tu. Bure kabisa tunafanya mhimili ule unaoneka kama…,kwa sababu ya sheria moja ama tatu ambazo busara ya kawaida isingeziruhusu kupita,” amesema.

Pia amewataka mawaziri kuwa na tabia ya kujipima wenyewe utendaji wao wa kazi badala ya kusubiri kupimwa na watu wengine.

Amesema katika miaka aliyokaa bungeni ameshuhudia mawaziri wasioshaurika na mara kadhaa wanaelezwa mambo na kamati za Bunge lakini hawasikii.


“Hata kwa jambo ambalo liko wazi tu lakini haambiliki hayo tumeyaona lakini sidhani kama nyie mtakuwa sehemu ya hao. Wanadamu wenzako wakikushauri wakarudia tena tena jaribu kuchunguza,” amesema.

Ameeleza kuwa si vizuri wabunge wakianza kumsema waziri kuwa haambiliki kwa sababu wataacha kukwambia na kukushauri na kuwataka kumsaidia rais kwa vitendo huku akianika kwamba ukiona rais amelaumiwa sana mtaani ni kwa sababu mmoja wa mawaziri hajawajibika ipasavyo.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3mrpx6K
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story