Kocha Nabi Athibitisha Bangala, Yakouba na Muloko Kuikosa MBEYA United, Aucho Mguu Ndani Mguu Nje


Licha ya kuwa kikosini kuendelea na mazoezi ya pamoja na timu kiungo wa Yanga, Khalid Aucho huenda akawa miongoni mwa nyota watakaokosa mchezo wa leo dhidi ya Mbeya Kwanza katika Ligi Kuu ya NBC.

Akizungumza jana Novemba 29, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi, amesema Aucho bado haijaeleweka rasmi kama atakuwa kikosini kwa wachezaji watakaocheza mechi hiyo kutokana na kutopona vizuri majeraha lakini hali ya uwanja pia.

Amesema kuwa wachezaji wengine ambao watakosekana leo uwanjani ni Yanick Bangala mwenye kadi za njano na Yacouba Sogne aliyeumia goti na Jesus Moloko aliyeumia sehemu ya ubavu wakati wa mazoezi.

“Yanga ni kubwa kwahiyo kukosekana kwa mchezaji mmoja kunawapa wengine nafasi kuonesha uwezo wao, kimsingi tumejipanga kushinda mechi hiyo na tunajua ushindani utakuwepo” amesema Nabi.

Kocha huyo ameongeza kuwa mipango yao msimu huu ilikuwa ni kushinda mechi zote, lakini mchezo uliopita dhidi ya Namungo walishindwa kufikia malengo kwa kuambulia sare huku akidai kuwa hawajakata tamaa.

Ameongeza kuwa maandalizi ya mechi ya leo ni tofauti na mchezo uliopita kwani Namungo ni tofauti na Mbeya Kwanza sambamba na hali ya uwanja ni tofauti.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/31aZXLr
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI