Mwanamke aliyepanga kusafiri Saudia kwa ajili ya Umrah akamatwa akiwa na Cocaine Abuja
Shirika la kupambana na madawa ya kulevya nchini Nigeria (NDLEA) limesema kuwa limemkamata mwanamke aliyekuwa njiani kuelekea nchini Saudia kwa ajili ya Umrah akiwa na mifuko 80 ya cocaine katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Abuja.
Mshukiwa, huyo Adisa Afusat Olayinka, mzaliwa wa jimbo la Kwara, ambaye amekuwa akiishi eneo la Ibafo katika eneo la Ogun, alikamatwa alipokuwa ndani ya Qatar Airways flight, imesema taarifa ya NDLEA, Jumatatu.
Mwanamke huyo amesema kuwa alianza kujihusisha na usafirishaji wa mihadarati baada ya kukutana na mwanamke mwingine katika Umrah katika mwaka 2019.
Hatahivyo, kulingana na taarifa, mwanamke huyo alisema alikuwa anataka kuchangisha Naira milioni 7 ili kuweza kutibiwa ili apate mtoto baada ya kuolewa kwa miaka 28 bila mtoto.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3pfnaE3
via IFTTT
Comments
Post a Comment