Safari ya Harmonize Kutoka WCB Lazima Uwe na Moyo Mgumu Kama Chuma



Kesho tarehe 5/11 ni siku rasmi ambayo msanii @harmonize_tz anaachia albamu yake ya pili, HIGH SCHOOL, si kitu rahisi kama msanii aliyeachana na Label yenye fan base kubwa na kuamua kujitegemea na kufanya yote haya ndani ya muda mfupi,ikiwemo kuanzisha Label, kufanya albamu mbili na kusimamia wasanii wengine.

Ishu ya Harmonize kujulikana kama Sio msanii tena wa WCB, iliwekwa hadharani kwa mara ya kwanza na Meneja Sallam SK August 21,2019 kwenye kipindi cha BLOCK 89, Wasafi FM. Nikimnukuu, Sallam alisema...👇

“Harmonize kwa sasa hivi ndani ya moyo wake hauko WCB, Harmonize kimakaratasi bado yuko WCB. Kwanini nasema hivyo, Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya kuterminate mkataba wake na yuko willing kupitia vipengele vyote vya sheria kuweza kuterminate mkataba wake.

Ni kitu ambacho tumependezewa nacho na yeye ameridhia ,ameomba kikao na uongozi,tunafurahi amefwata sheria na tunaachana salama”- Sallam SK.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3DfhjUm
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI