Serikali kutunga sheria ya kuboresha usafiri wa umma nchini



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Ummy Mwalimu
Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema itatunga sheria mahususi ya kuboresha usafiri wa umma kwenye miji yote nchini.

 Hayo yamesemwa leo Jumanne Novemba 30, 2021 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali (Tamisemi), Ummy Mwalimu wakati akielezea mafanikio ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Amesema kumekuwepo kwa ongezeko kubwa la watumiaji wa huduma bora ya usafiri wa umma kwa Mkoa wa Dar es Salaam na hata miji mingine ya Tanzania.

Amesema mfano mahitaji ya usafiri wa umma na miundombinu bora ya watembea kwa miguu ni asilimia 84 (Dar es Salaam), asilimia 80 (Dodoma), asilimia 90 (Mwanza), asilimia 70 (Arusha), asilimia 87 (Tanga), na asilimia 70 kwa Mkoa wa Mbeya.


 
“Mwelekeo baada ya miaka 60 ya uhuru ni kutunga sheria mahususi ya kuboresha usafiri wa umma kwenye miji yote ya Tanzania kupitia miundombinu na huduma zilizoratibiwa,”amesema.

Kuhusu Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Jiji la Dar es Salaam (DART), Waziri Ummy amesema mradi huo umepunguza muda wa safari toka saa tatu kabla ya kuanza mradi hadi wastani wa dakika 45 kwa safari moja.

Amesema hilo limewawezesha wananchi kuwahi katika shughuli zao za kijamii na kiuchumi zinazoongeza tija kwenye Pato la Taifa.

Aidha, amesema kumekuwa na ongezeko la watumiaji wa usafiri wa umma kupitia mradi wa huo kutoka abiria 76,000 kwa siku wakati mradi ulivyoanza kutoa huduma Mei 2016 hadi kufikia abiria 200,000 kwa siku mwaka 2018.

Hata hivyo, amesema baada ya kupata changamoto za kiundeshaji idadi hiyo kushuka hadi wastani wa abira 100,000 kwa siku mwaka 2020 na kwamba baada ya maboresho yanayoendelea, hivi sasa wastani wa abiria ni 160,000 kwa siku.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3d6uEnp
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI