Ubalozi wa China nchini Uganda wafunguka kuhusu ripoti za Uwanja wa Ndege wa Entebbe




Ubalozi wa China nchini Uganda umejibu kuhusu ripoti kwamba Uganda inajiingiza kwenye hatari kwa kuutoa Uwanja wa Ndege wake wa Kimataifa wa Entebbe na kuupa China, kutokana na mkopo wa dola milioni 200 za Kimarekani (sawa na Ush713 billion). Kiasi hicho kilipatikana kupitia makubaliano yaliyosainiwa Machi 31, 2015 kati ya serikali ya Uganda na benki ya Usafirishaji na Uagizaji ya China (Exim). Hivyo msemaji wa ubalozi wa China nchini Uganda, Bw. Fang Yi, amesema ushirikiano kati ya China na Uganda siku zote unafuata misingi na kanuni za uwazi, usawa, na kunufaishana pande zote mbili. Na katika makubaliano hakuna masharti yoyote ya kawaida au ya kisiasa yaliyoambatanishwa.

Kwa upande wake serikali ya Uganda pia imekanusha ripoti hizo, ambapo kwa mujibu wa Waziri wa habari Dkt Chris Baryomunsi, ambaye ni msemaji wa serikali, hizo ni habari za uwongo na kusisitiza kuwa serikali haiwezi kutoa mali ya taifa kama uwanja wa ndege.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3FXkCBk
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI