Joyce Kiria Aonekana Mwenye Furaha Sana ndani ya Penzi Jipya Baada ya ndoa zake Mbili Kuvunjika

 


Joyce anaonekana mwanamke anayejali sana pale anapopenda, ila huwa kile kinachotokea baadae huwa nje uwezo wake. Sababu ya uwazi wake Mahusiano yanapoanza kuyumba huwa hakuna siri. Na sio kwamba huyaacha mahusiano yavunjike hivihivi. Huwa anapambana lakini sababu hamna anachoweza kubadili hishia kuvunjika moyo, kuugulia hadi anapoibuka tena na kitu kipya

Achilia mbali mateso aliyosema aliyapata hadi kuachana na mumewe wa kwanza yule DJ Nelly, Joyce ameonekana kuwa mwanamama mkweli na muwazi anapokuwa kwenye mahusiano na hata pale yanapovunjika.

Haijalishi nini itakua hatma ya mahusiano yake ila Joyce ni aina ya wale wanawake ambao akipendwa anataka ulimwengu wote ujue kwamba anapendwa na amepata mtu sahihi kwa wakati ule na ana furaha.

Nakumbuka wakati siasa za chadema zimeshika kasi Tanzania aliyekua mume wa Joyce Henry Kileo akawekwa ndani Joyce alivyopambana kumnusuru, tena akiwa na watoto wadogo.

Hata kwenye kampeni za ubunge kule Mwanga Joyce alipambana kwelikweli kumsaidia mumewe

Baadae Joyce alitumbukiwa nyongo baada ya kugundua pamoja na yote yale aliyokua anayafanya Kileo alikua akimsaliti kwa kuwa na wanawake ndani ya chama chao huku akiwa mkali kwa mkewe, kuacha kufanya majukumu ya kutunza familia na kumpa kipigo pale alipokuwa anaulizwa.

Tangu ameachana na Kileo amekua kimya sana ila sasa amekuja na kitu kipya, anaonekana mwenye furaha na shemela ameweza kuyafuta maumivu yote na upweke aliokua anapitia Joyce. Kikubwa zaidi amebeba watoto wa Joyce kama wa kwake

Mimi binafsi nawatakia Joyce na Aaron furaha ya milele kwenye mahusiano yao

Hatimaye watoto wa baba mzazi Kileo wamepata baba mlezi.

Haki wababa nyie mna kila sababu ya kupambana ili muwalee watoto wenu.... Ndoa isingevunjika Kileo angekua anawalea watoto wake

Mungu sadia wadumu maana Likitokea la baya watakaoathirika sio wao tuu, hata watoto wao wataumia

By Mama D/JF




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3eE459X
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI