Kagere, Wawa, Banda wavunjiwa mikataba Simba



KLABU ya soka ya Simba imevunja mikataba ya nyota wake wanne wa kigeni wakiwemo mastaa wao aliokuwa tegemeo katika kikosi hicho kwa misimu kadhaa, beki wake Raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa na mshambuliaji wake, Mnyarwanda, Meddie Kagere. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Mbali na mastaa hao wawili tegemeo, nyota wengine wa kimataifa waliotemwa ni Peter Banda aliyesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili mwezi Agosti na kiungo mshambuliaji Dancan Nyoni Raia wa Malawi ambaye ameshindwa kuonesha makali yake toka asajiliwe klabuni hapo.

Simba imeamua kuvunja mkataba na wachezaji hao, ili kupata nafasi ya kusajili wachezaji wengine wa kigeni kwenye dirisha dogo la usajili.


Pascal Wawa
Ikumbukwe hivi karibuni klabu hiyo ilivunja mkataba kwa makubaliano maalumu na kocha wake msaidizi Thiery Hitimana raia wa Burundi.


 
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameamua kufanya maboresho kwenye kikosi chao kufuatia kusuasua hivi karibu.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3EHTOEd
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI