Ndoa ya Dida SHAIBU Iko Shwari Ajaachwa Wala nini, Muheshimiwa Meya Athibitisha

 


June 10 mwaka huu,watu walianza maisha rasmi ya ndoa kati ya mtangazaji maarufu nchini wa kipindi cha mashamsham cha Wasafi Fm, @didahshaibutz pamoja na Diwani wa Vingunguti na Meya wa jiji la Dar es salaam,mh. Omary Kumbilamoto.

Huku na huku hivi karibuni wambea wakanasa ubuyu kuwa wawili hao wamepeana kikono,mh! ni mapema sana mjue,maneno kibao kwa Dida kuwa ana nyota ya kaniki,haeleweki msafi ama mchafu, ndoa zote za bando.

Hasa kupitia U-HEARD ya XXL na @soudybrown , Mh. Kumbilamoto ameweka sawa kuwa ndoa yao ipo na inanoga kila leo, wao pia wanaona tu maneno mitandaoni na wanayazika. Mbali na Mh., shemeji mtu (kaka wa Dida) alikuwa ofisini kwa shemeji yake (sijui alikuwa anachezesha mzinga wa sikukuu) akapewa mkonga na Kumbilamoto na kuthibitisha kuwa hata wao wanashangaa mahasidi wa penzi la Dida, maana penzi lilivyo, ndoa kama imefungwa leo hata Honeymoon bado.

Uheaard....



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3sPJ98l
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI