Okwi, Aucho watoswa Uganda Cranes



KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’, Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameita kikosi cha wachezaji 23, kitakachoingia kambini kwaajili ya michezo ya kimataifa dhidi ya Gabon Desemba 30 na Mauritania Januari Mosi.

Katika kikosi hicho Kocha Micho amemuita kiungo Chris Pius Akena, kikosini

kwa mara ya kwanza huku Khalid Aucho wa Yanga na Emmanuel Okwi anayecheza Kiyovu ya Rwanda wakiachwa.

Akena anayecheza katika kikosi cha Ahly Shabab FC, ambacho kinashiriki Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu (UAE) amewashtua wengi baada ya kuitwa na kocha Micho.


 
Akena ni miongoni mwa wachezaji watatu walioitwa mapema kikosini pamoja na kiungo wa URA, Shafik

Kuchi Kagimu na nahodha wa BUL George Kasonko.

Nyota huyo wa zamani wa Maroons, aliyekulia katika kituo cha kukuzia vipaji cha Pro-Way Soccer Academy chini ya usimamizi wa Aspire kutoka nchini Qatar alijiunga na Ahly Shabab Januari mwaka huu.


Kiungo huyo tayari ameshinda taji la UAE Pro League akiwa katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 cha Ahly Shabab.

“Akena ni mchezaji mzuri baada ya mafanikio aliyoyapata akiwa UAE tumeamua kumuita katika michezo hii miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Gabon na Mauritania. Lakini pia tumemuita Shafik Kagimu na George Kasonko kukamilisha idadi ya wachezaji 23,” alisema Micho.

Micho amewarejesha kikosini Mohammed Shaban, Patrick Kaddu, na Makinda Juma, Jack Komakech (kipa) wengine ni Travis Mutyaba, (kipa) Isma Watenga na kiungo Moses Waiswa.

Kikosi hicho kinaundwa wa makipa, Isma Watenga (Chippa United, Afrika Kusini), Joel Mutakubwa (Express) na Jack Komakech (Vipers)

Mabeki ni Enock Walusimbi (Express), Gavin Mugweri (SC Villa), Abdulazizi Kayondo (Vipers), Juma Ibrahim (KCCA), Halid Lwaliwa (Vipers), Najib Fesali (URA) na Kenneth Semakula (SC Villa).

Viungo ni Chris Akena (Ahly Shabab, UAE), Moses Waiswa (Supersport United, Afrika Kusini), Kizza Martin (Express FC), George Kasonko (BUL), Shafik Kagimu (URA), Bobosi Byaruhanga (Vipers SC), Mahad Kakooza (Express).

Washambuliaji ni Yunus Sentamu (Vipers), Ibrahim Orit (Vipers SC), Travis Mutyaba (SC Villa), Patrick Kaddu (hana timu), Steven Desse Mukwala (URA), Mohamed Shaban (Onduparaka).


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3EAZNui
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI