Rafiki wa Jana Ndie Adui Mkubwa Kesho, Makundi Kombe la Shirikisho Africa Yapangwa, Chama Uso Kwa Uso na Simba


Klabu Ya Simba inatarajia kukutana na kiungo wake wa zamani, Clatous Chama baada ya kupangwa kundi D na  RS Berkane ya Morocco, hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika


Mbali na Chama ndani ya kikosi hicho, pia Simba itakutana na winga wa zamani wa Yanga, Tuisila Kisinda. Chama aliuzwa na Simba katika klabu ya RS Berkane, ingawa hivi karibuni kulikuwepo na tetesi za kumrejesha ndani ya kikosi hicho cha Msimbazi, hivyo mashabiki watamshuhudia kupitia michuano hiyo ya Caf.


Simba inashiriki michuano hiyo, baada ya kuanguliwa Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo iliangukia  michuano ya Kombe la Shirikisho, ambapo ilicheza na  Red Arrows ya Zambia na kuitoa kwa jumla ya mbao 4-2, ushindi uliwapeleka makundi.

Simba imepangwa kundi D na RS Berkane, Asec Mimosas na Us Gendarmerick National.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3z55NdT
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI