Hii ndiyo tofauti kati ya WCB Wasafi na Konde Music



Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa mashabiki wamekuwa wakizishindanisha lebo za WCB Wasafi na Konde Music Worldwide kutokana na ushindani wa wamiliki wake katika Bongofleva.

WCB Wasafi iliyomtoa Harmonize kimuziki mwaka 2015 ni ya Diamond Platnumz.

Baadaye Harmonize alianzisha Konde Music na hapo ndipo ushindani ukaibuka. Hata hivyo, ukweli ni kwamba lebo hizi zina tofauti kubwa katika baadhi ya mambo kama ifuatavyo;

1. Hadi sasa WCB imefanikiwa kutoa albamu tatu na Extended Playlist (EP) nne za wasanii wake sita, huku Konde Music ikitoa albamu moja na EP tatu za wasanii wake wanne.


 
2. Konde Music imefanikiwa kumsaini msanii kutoka nje ya Tanzania, Young Skales (Nigeria) lakini WCB haijafanya hivyo, licha ya kuwapo taarifa za kufungua tawi lao Kenya.

3. Kwa sasa WCB inasimamia wasanii sita ambao ni Diamond, Rayvanny, Queen Darleen, Lava Lava, Mbosso na Zuchu, huku Konde Music ikisimama na wasanii sita ambao ni Harmonize, Ibraah, Young Skales, Cheed, Killy na Angella.

4. Tayari wasanii wawili wamejiondoka WCB, akiwamo Rich Mavoko (2018) na Harmonize (2019), huko Konde Music akiondoka msanii mmoja, Country Boy (2022).


5. Konde Music ilizaliwa baada ya Harmonize kuondoka WCB iliyomtoa kimuziki, wakati WCB ilizaliwa baada ya Diamond kuondoka Sharobaro Records iliyomtoa pia na yeye kimuziki.

6. Hadi sasa hakuna msanii aliyesainiwa chini ya Konde Music aliyeshinda au kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa, lakini WCB wasanii wake Rayvanny na Zuchu wamefanikiwa kwa vyote.

7. Tayari Diamond ameshafanya kolabo na wasanii wote aliowasaini WCB kama sehemu ya kuwatangaza zaidi, lakini Harmonize bado hajafanya hivyo kwa msanii wake mmoja wa Konde Music, naye ni Cheed.

8. WCB imetoa nafasi kwa msanii wake Rayvanny kuanzisha lebo yake, Next Level Music (NLM), lakini Konde Music bado hakuna msanii aliyefanya kitu kama hicho, licha ya Harmonize kudokeza kuwa Ibraah anaweza kuwa na lebo yake.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/SVl6QGNOM
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI