Maduka 16 ya Wafanyabiashara wa soko Mkoani Geita yameungua kwa moto


Maduka 16 ya Wafanyabiashara wa soko la CCM kakubilo lililopo Wilaya ya Geita Mkoani Geita yameungua kwa moto na kuteketea kwa moto ambao hadi sasa bado chanzo chake hakijajulikana.

Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Geita, Wilsoni Shimo imefika katika eneo hilo na kujionea hali halisi huku maduka 16 yakiwa yameungua na baadhi ya vitu kuibiwa.


Aidha Shimo ameliagiza Jeshi la polisi kwa kushirikiana na uongozi wa soko hilo pamoja na Viongozi wa kata kuahakikisha wanashirikiana kuwasaka wote waliokwenda kutoa msaada na kuiba mali ambazo zilikuwa hazijateketea.


"Mwenzio alitarajia umekuja kuchukua zile nguo ambazo hazijaungua moto uzitunze mahala uumpe lakini wewe zile nguo unachukua unapeleka unakojua wewe mwenyewe huo ni wizi tabia hii na hii roho sio nzuri sana si jambo jema na huo si utanzania wetu ni bora hii tabia ikafichuliwa" ——— Shimo, Mkuu wa wilaya.


from UDAKU SPECIAL https://bit.ly/3rXyLJC
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI