UTEUZI: Raos Samia Afeua Vigogo Hawa Serikalini





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao: -

1. Amemteua Prof. Ulingeta Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya

Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE). Prof. Mbamba anachukua nafasi ya Dkt. Ng'wanza Kamata Soko

aliyemaliza muda wake.

Prof. Mbamba ni Profesa Mshiriki na Amidi wa Shule Kuu ya Biashara,

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

2. Amemteua Bi. Zuhura Sinare Muro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Bi. Muro ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ushauri Elekezi ya Kazi Service Limited na Mkufunzi wa muda katika Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute), Dar es Salaam.

3. Amemteua Prof. Leonard James Mselle kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya TEHAMA.

Prof. Mselle ni Mhadhiri, Rasi Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu

Angavu, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Uteuzi huu unaanza tarehe 29 Januari, 2022.


UTEUZI: Raos Samia Afeua Vigogo Hawa Serikalini


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/CkEV8KOLs
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI