Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Mtibwa vs Yanga"



1: STILL UNBEATEN.. YANGA ISIYOFUNGIKA✊ Tamu redioni. Tamu gazetini. Tamu mitandaoni. Tamu kiwanjani🙌 Ile ndio YANGA TAMU iliyoimbwa na Marioo..

2: Haikuwa Perfomance ya kushitua sana Lakini umekuwa ushindi mkubwa, wa kibabe, kufungia mzunguko wa kwanza wa Ligi katika Uwanja wa Kibabe.. Kabla ya Yanga kuwasili, Mtibwa ilikuwa haijawahi kufungwa bao katika mechi 3 walizocheza Manungu!

3: Hongera kwa Profesa Nabi👏 Katika mahojiano ya mwanzo wa mchezo, Cedrick Kaze alionyesha ni jinsi gani benchi la ufundi la Yanga lilifanya kazi nzuri kujiandaa na mchezo huu! Tactically, Hoja ya size ya uwanja wa Manungu iliendana vyema na 'selection' ya wachezaji. Kivipi?

4: Unahitaji Ball Players zaidi kiwanjani kwa ajili ya kuutunza mpira na kuwa na maamuzi ya haraka pindi wanapoiba mpira.. Sure Boy, Feisal, Aucho na Ntibazonzika waliwapa Yanga umiliki mzuri wa mchezo Yanga katika eneo la katikati ya kiwanja

5: SAIDO NTIBAZONKIZAA.. 🙌 MAN ON FORM🔥 Sema yote kuhusu mbinu za NABI na Benchi Lake Lakini mwisho AKILI KUBWA ya mpira ya Saido imewapa Yanga heshima kubwa pale Manungu.. What A Player. What A Perfomance

6: Mtibwa ni kama walipanga kuwakaba Yanga katika mstari wa juu Lakini walikosa 'organaization' nzuri kwenye Plan hiyo. Timu ilitawanyika sana muda walipopoteza mpira

7: Juma Nyangi.. Naelewa sana ubora wake Timu ikiwa na mpira Lakini bila mpira sidhani kama ana sifa za kutosha kuwa kiungo wa chini.. Nafikiri ndio kitu Mtibwa walikikosa katikati ya kiwanja. Sio Ndemla, Chota wala Nyangi mwenye quality ya kupokonya mpira

8: WELL DONE REFA JOACHIM AKAMBA na Wasaidizi wake.. 👏 Tunaona matunda ya Semina! Umuhimu wa 'mawasiliano mazuri' kwa Waamuzi umepelekea kuamua vizuri tukio la Fei Toto.. NI KWELI FEI ALISHIKA

9: Yanick Bangala.. Mtu dume haswa! Mzuri hewani. Mbabe ardhini.. Na bado ni msaada mkubwa kwa Yanga wanapoanzisha shambulizi..

10: Kipa Diarra kuna kitu anatakiwa kukiboresha.. Anapoteza sana umakini langoni. Iko siku Top Striker watatumia hilo kumuadhibu.. Asante Farid Mussa

Nb: Baridi la Afrika vs Baridi la Tanzania.. Nani ana enjoy sana..? 😃  


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/F6g5ky7
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI