Hatimaye Kundi la Watanzania 20 Ambalo Limekuwa Barabarani kwa zaidi ya saa 40 Lavuka Mpaka wa Ukraine


Hatimaye Kundi la Watanzania 20 ambalo limekuwa barabarani kwa zaidi ya saa 40 likikimbia vita nchini Ukraine limefanikiwa kuvuka mpaka wa Ukraine na kuingia nchini Poland dakika chache zilizopita.

Mmoja wa Watanzania hao aitwae Nenyoratah Teveli ameiambia @AyoTV_ kwamba kwa leo tu kwenye safari ya kuutafuta mpaka ilibidi watembee kilometa 26 kwa mguu hadi kufika mpakani hapo baada ya barabara kuzibwa na foleni kubwa ya magari ya wanaokimbia vita hiyo.

Wengi wa Watanzania nchini Ukraine ni Wanafunzi katika vyuo mbalimbali wakisomea kozi mbalimbali ikiwemo udaktari na hadi sasa bado kuna Watanzania wengine wako kwenye miji mbalimbali ya Ukraine katika harakati za kukimbilia mpakani ili kuiacha Nchi hiyo, endelea kukaa karibu na @millardayo kwa updates zote.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/1MbqyVk
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI