Majeshi ya Urusi Yautwaa Mjii Mkuu wa Ukraine.....Rais Watakakiwa Kujihami



Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametia saini agizo la kuwataka wananchi wake wajiandae kwa ajili ya ulinzi. Agizo hilo litatekelezwa kwa muda wa miezi mitatu. 

Kwa mujibu wa taarifa raia pamoja na jeshi la akiba wanaandikishwa kwa ajili ya kuilinda nchi yao kutokana na uvamizi wa Urusi. 


Wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 60 sasa hawaruhusiwi kuondoka nchini. Wakati huo huo majeshi ya Urusi tayari yameshaingia nchini Ukraine na yako mbele ya mji mkuu wa nchi hiyo Kiev. 


Afisa mmoja wa ujasusi wa nchi ya magharibi ameliambia shirila la habari la AFP kuwa Urusi sasa inaidhibiti anga ya Ukraine. 


Nchi hiyo sasa haina tena jeshi la anga la kuilinda.Kwa mujibu wa taarifa ya afisa huyo wa ujasusi, Urusi itaingiza idadi kubwa ya askari karibu na mji mkuu katika muda wa saa zijazo. 


Mpaka sasa watu wapatao 137 wameshauawa kutokana na mashambulio ya ndege na ya majeshi ya ardhini yaliyofanywa kwenye sehemu kadhaa za Ukraine. 


Taarifa zaidi zinasema majeshi ya Urusi yameshauteka uwanja wa ndege wa jeshi la Ukraine pamoja na kinu cha nyuklia cha Chernobil kilichopatwa na ajali mnamo mwaka 1986.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/1w0kEDL
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI