Rapper Maarufu Nchini Afrika Kusini Almaarufu ‘Riky Rick’ Amekufa Baada ya Kujinyonga
Rapper maarufu nchini Afrika Kusini, Rikhado Muziwendlovu Makhado almaarufu ‘Riky Rick’ amekufa baada ya kujinyonga jijini Johannesburg.
Muda mfupi kabla ya kuchukua uamuzi wa kujinyonga, kupitia ukurasa wake katika akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter, Riky aliandika: “I’ll return a stronger man. This land is still my home,” akimaanisha ‘Nitarejea nikiwa na nguvu zaidi. Nchi hii bado ni nyumbani kwangu!
Familia ya msanii huyo, imethibitisha kutokea kwa tukio hilo, leo, Jumatano Februari 23 na kueleza kwamba amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 34 na kueleza kwamba ameacha pengo kubwa kwa familia kwani ilikuwa ikimpenda na kumtegemea.
Bado haijafahamika ni nini kilichomfanya msanii huyo akachukua uamuzi huo ambapo familia imeomba iachwe iomboleze kwa amani katika wakati huu mgumu na kwamba ratiba za mazishi zitatolewa baadaye.
Mwanamuziki huyo, alipata umaarufu mwaka 2014 baada ya kutoa ngoma yake ya Nafukwa na baadaye akatoa albamu iitwayo Family Values iliyotunukiwa hadhi ya mauzo ya Platnum na RiSA.
Mwaka 2019 alianzisha Tamasha la Muziki wa Hip Hop la Cotton Fest na mwaka huu, tamasha hilo lilikuwa likitarajiwa kufanyika kuanzia Machi 19 hadi Machi 20.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/yLMunxb
via IFTTT
Comments
Post a Comment