Simba Yachapwa, Yashuka Hadi Nafasi ya Pili
KLABU ya Simba imekubali kipigo cha 2-0 dhidi ya RS Berkane katika mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa nchini Morocco.
Mabao ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Adama Ba na Charki El Bahri yameifanya Berkane watoke na pointi tatu muhimu.
Ushindi huo unaifanya Berkane washike nafasi ya kwanza katika kundi D wakiwa na pointi sita huku upande wa Simba wao wakishika nafasi ya pili wakiwa na utofauti wa magoli na USGN wanaoshika nafasi ya tatu huku wote wakiwa na pointi nne.
Katika kipindi cha kwanza dakika 32 Berkane walifunga bao na Adama Ba ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua ukurasa wa mabao akitumia vizuri mpira wa adhabu (Faulo) dakika 32 akipiga na kwenda wavuni moja kwa moja.
Mshambuliaji huyo alitaka kufunga bao la pili dakika 39 baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kuoiga shuti kali lakini beki wa Simba, Kennedy Juma aliwek kichwa na mpira ulimgonga na kuwa kona.
Simba washambuliaji wake walionekana kutokuwa na mipango ya kupenya safu ya ulinzi hali iliyowafanya washindwe kupiga hata shuti moja mlangoni.
Dakika 41 Charki El Bahri aliifungia Berkane bao la pili kwa kichwa akitumia vizuri kona iliyopigwa na Badri.
Katika kipindi cha pili Simba walianza kwa kufanya mabadiliko ya kumtoa Peter Banda na kuingia Benard Morrison ili kwenda kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji.
Berkane nao walianza kwa presha kubwa na dakika 46 beki wa Simba, Joash Onyango alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Najji Larrbi.
Dakika 50 Aishi Manula alifanya kosa baada ya kushindwa kupiga mpira mbele na mshambulliaji wa Berkane, Charki El Bahri aliuwahi na kupiga shuti dogo lakini mpira ulienda nje.
Dakika Berkane walitaka kufunga bao la tatu baada ya Tuisila Kisinda kumtoka beki wa Siba, Henock Inonga na kupiga pasi kwa Hamza El Moussaoui aliyepiga shuti na Manula aiucheza na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda kwa Berkane.
Mabadiliko ya Simba kwa kuingia Morrison yalionekana kuwa na tija kwani mchezaji huyo alikuwa anapeleka presha langoni kwa Berkane.
Morrison alikuwa anakaa na mpira huku muda mwingine akilazimisha kupenya safu ya ulinzi ya wapinzani.
Dakika 63 Simba ilikosa bao baada ya kupata mpira wa adhabu (Faulo) iliyochongwa na Morrison kisha Sadio Kanoute alionganisha kwa kichwa mpira ukagonga mwamba na mabeki wa Berkane wakaokoa.
Berkane walifanya mabadiliko dakika 66 wakimtoa Adama Ba na kuingia Mohamed Farahane na dakika 76 wakamtoa Hamza El Moussaoui na nafasi yake aliingia Mohamed Aziz, Shadrack Mzungu na kuingia Moudad Fakak huku Simba akitoka Sadio Kanoute na kuingia Jimmyson Mwanuke.
Morrison alionyeshewa kadi ya njano dakika 86 baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Berkane.
Pablo alifanya mabadiliko mengine dakika 89 akimtoa Ousmane Sakho na kuingia Yusuph Mhilu mabadiliko ambayo yalionekana kutokuwa na tija.
Mpaka mpira unamalizika Simba walionekana kuzidiwa mipango na Berkane ambao walitawala mchezo huo kwa dakika zote 90.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/JUF2D3P
via IFTTT
Comments
Post a Comment