Urusi Inatumia Trilioni 46 kwa Siku Kuikabili Ukraine



Wachambuzi wa masuala ya vita, wameeleza kwamba Serikali ya Urusi, inatumia takribani paundi bilioni 15 ambazo ni takribani trilioni 46 za Kitanzania kwa siku katika vita dhidi ya Ukraine.
Licha ya kiwango hicho kikubwa mno cha fedha zinazotumika, wachambuzi mbalimbali wanaeleza kwamba bado Urusi haijafanikiwa katika uvamizi wake na endapo Ukraine itaendelea kuleta upinzani mkali kwa siku kumi zijazo, uchumi wa Urusi utaporomoka vibaya.

Afisa wa Shirika la Ujasusi la Uingereza, M16, Richard Moore ameonya kwamba huenda Urusi ikashindwa vibaya kwenye vita hivyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kujiamini kupita kiasi, kuidharau Ukraine, bajeti kubwa inayotumia kwa simu na ujasiri wa Ukraine wanaouonesha kwenye vita hiyo.

Katika tamko lake alilolitoa, Moore amesema haamini kama Rais Vladimir Putin atashinda katika vita hiyo kutokana na umoja na mshikamano unaooneshwa na wanajeshi wa Ukraine pamoja na raia wake huku wananchi wengi wa Urusi wakionesha kuchukizwa na hatua ya rais wao kuivamia Ukraine.

Wakati hayo yakiendelea, tayari Ukraine imeanza kupata uungwaji mkono kutoka mataifa mbalimbali ambapo Rais Joe Biden wa Marekani, ameidhinisha kiwango cha dola milioni 350 za Kimarekani kama msaada kwa Ukraine kupambanana Urusi katika vita hiyo.


 
Lakini pia tayari Ujerumani imetoa msaada wa vifaru 400 na silaha nyingine kwa ajili ya kulisaidia Jeshi ya Ukraine kupambana na uvamizi huo wa kimabavu.

Mataifa mengine yaliyojitokeza kuisaidia Ukraine, ni jamhuri ya Czech ambayo imetoa silaha zinazokadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 6.4 kwa serikali ya Ukraine huku Canada, Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya wakitangaza kuiondoa Urusi kwenye mtandao wa kimataifa wa kibenki, maarufu kama Swift.

Jeshi la Kujihami la NATO, nalo limeahidi kutuma kikosi chake haraka iwezekanavyo nchini Ukraine kuisaidia nchi hiyo kupambana na uvamizi wa Urusi.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/mQGWT8I
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI