Kauli Yamponza...Kamanda wa Polisi Aliyeomba Kuteuliwa na Rais Kuwa IGP Arudishwa Makao Makuu Kwa Uchuguzi




Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro leo Machi 29, 2022 amefanya uhamisho na mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa. Katika uhamisho huo, aliyekuwa RPC Mkoa wa Kagera, ACP Wankyo Nyigesa amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa RPC Rukwa, ACP William Mwampagale.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, uhamisho huo umefanyika ili kupisha uchunguzi wa tukio la tarehe 26.3.2022 katika sherehe ya kumuaga ACP Wankyo ambapo alitoa maneno ambayo yanaonyesha kuwepo na ukiukwaji wa nidhamu kulingana na miongozo ya Jeshi la Polisi.

Pia katika mabadiliko hayo, Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Rukwa, ACP Theopista Mallya anakuwa RPC wa mkoani Rukwa aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Rukwa, ACP Mashenene Mayila anakuwa Afisa Mnadhimu wa mkoa huo.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/MefoCkF
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI