Mungu Tusaidie..Ajali Nyingine Mbaya Yaua WATU Sita Asubuhi ya leo


Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari (fuso) lenye namba T 239 AFB walilokua wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika eneo la barabara ya Soni/Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Akizungumza na @ayotv_ kwa njia ya simu RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo March 29,2022.

Aidha Kamanda Jongo amewataka Watumiaji wa vyombo vya Moto mkoani humo kuendelea kufuata sheria,kanuni na taratibu za usalama barabarani.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto na majeruhi wapo Hospitalini hapo wakiendelea kupata matibabu.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/DRld1Lv
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI