Ramadhan Kabwili Afichua SIRI nzito Young Africans

 


Mlinda Lango Ramadhan Kabwili amevunja ukimya na kueleza kwa undani ukweli wa maisha yake baada ya kushindwa kuonekana kwenye kikosi cha Young Africans msimu huu 2021/22, huku ikielezwa aliachwa mwishoni mwa msimu uliopita.


Kabwilia mbaye kwa kipindi kirefu alikua kimya amesema wadau wengi wa Soka la Bongo wamekua hawafahamu kinachoendelea kati yake na Uongozi wa Young Africans, lakini ukweli ni kwamba bado ni mchezaji halali wa klabu hiyo.


Mlinda Lango huyo aliyekua sehemu ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17 kilichoshiriki Fainali za Afrika 2017 nchini Gabon, amesema ni kweli hayupo kwenye kikosi cha Young Africans kwa muonekano, lakini yupo klabuni hapo na anaendelea kulipwa mshahara wake kila mwezi.


“Naomba niweke wazi leo bado nipo Yanga, napokea mshahara wangu kwa wakati na posho kama ilivyo kwa wachezaji wengine,”


“Kiukweli nimeamua kuweka wazi kwa sababu sio jambo dogo viongozi wangu wanalifanya, sipo ndani ya timu kwa maana ya kufanya mazoezi ila nipo kimkataba lakini wananipatia kila kitu kwa wakati.”


Mkataba wangu na Yanga umebaki wa miezi minne na mwisho wa msimu huu ndio utamalizika baada ya hapo nitawafuata na kuwauliza wapo tayari kuendelea na mimi au nitafute changamoto mpya sehemu nyingine.” amesema Kabwili


Kabwili alisajiliwa Young Africans msimu wa 2017/18 kama mchezaji huru na aliwahi kuaminiwa klabuni hapo chini ya Kocha Mwinyi Zahera kufuatia Mlinda Lango Claus Kindoki wa DR Congo kushuka kiwango.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/C6FiZAP
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI