Vanessa Mdee Awajibu Mashabiki Wanaosema Amezeeka



Mwanamuziki Vanessa Mdee amewajibu mashabiki zake waliokuwa wanamtupia vijembe kwamba amezeeka.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mdee alisema kwamba kuzeeka ni baraka wala hajutii chochote.

"kuna Mtu kasema nishazeeka, kuzeeka ni faraja kwangu hilo sio tusi kabisa wala hata hunitingishi," Mdee alisema.


Mdee alishikilia kwamba la muhimu kwa sasa ni kuwa ana furaha katika maisha yake, hivyo kauli za watu hazina madhara yoyote kwake.

Baadhi ya mashabiki walisema kwamba tangu kichuna huyo aolewe na Rotimi, ameawiri sana na maisha yake yanazidi kuwa bora.

Wengine pia hawakusita kuibua stori za mpenzi wake wa awali, Juma Jux huku Vaessa akisema kwamba hayo ni mambo ya zamani na alishayasahau.

Alikuwa anayasema haya wakati akitambulisha rasmi programu yake na mumewe iitwayo Forthebetter.me ambapo shabiki anaweza kujisajili na kulipia kiasi kidogo cha pesa ili kupata burudai, makala mbalimbali, ushauri na kuuliza maswali kuhusu mastaa.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Ya4UJHB
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI