DC Sengerema Atoa Ufafanuzi Kisiwa Kinachodaiwa Kutembea




Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga akitoa ufafanuzi juu ya kisiwa kinachodaiwa kutembea wilayani humo
Sengerema. Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga amesema hakuna kisiwa kinachotembea kijiji cha Kahunda Kata ya Katwe wilayani humo bali ni kipande cha aridhi kilichomeguka na kuingia ziwani.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano April 27, 2022 alipokuwa akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake ili kutoa ufafanuzi juu kisiwa hicho.

Ametoa ufafanuzi huo baada ya wananchi kudai kuwa kisiwa hicho kilichopo katika kijiji cha Kahunda Kata ya Katwe kinatembea.

Ametoa rai kwa wananchi wanaokwenda ndani ya kipande hicho kuchukuwa tahadhari na kuwataka wataalamu wanaohusia na masuala ya aridhi pamoja na jiolojia kufika katika eneo hilo ili kitoa ufafanuzi zaidi.


Senyi amesema kuwa jana alikwenda katika kijiji hicho na kamati ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kujiridhisha juu ya taarifa hizo huku akisema kuwa waligundua hakuna kisiwa kinachotembea ndani ya ziwa Victoria.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/9PnBgvu
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story