Hatufanyi biashara ya binadamu - Rais Kagame

 

Rais wa Rwanda  Paul Kagame amesema kuwa nchi yake haifanyi biashara ya binadamu, ikiwa ni maoni yake ya kwanza toka nchi hiyo iingie makubaliano ya kupokea wahamiaji kutoka nchini Rwanda

Kwenye makubanliano yaliyoipo ni kwamba wahamiaji wanaosaka makazi ambao watawasili nchini Uingereza wakiwa kwenye boti ndogo, watapelekwa moja kwa moja nchini Rwanda.  


Mpango huo ambao Rwanda imepokea kiasi cha Paund milioni 120  sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania  bilioni 347,umekua ukikosolewa ndani na nje ya nchi hizo.   


Rais Kagame ambaye alikua na ziara katika nchi za Congo-Brazzaville, Jamaica, na Barbados wakati mpango huo ukitiwa saini amesema kuwa ni kosa kudhani kwamba Rwanda inanufaika na fedha kutokana na kupokea watu wanaosaka makazi.  


“hatuuzi binadamu  tafadhali, tuanawasadiia ” amesema Rais Kagame wakati wa semina chuo kikuu cha Brown nchini Marekani .


Rais Kagame amesema kwamba  Uingereza iliihitaji Rwanda kwa kwenye zoezi hili sababu nchi hiyo ina uzoefu wa kupokea wahamiaji hususani namna ilivyopokea  wahamiaji toka Libya.  


Ameongeza kuwa mwaka 2018 alipokua  mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwamba  Rwanda ipo tayari kuwapokea wahamiaji ambao wamekwama nchini Libya  ambao walikua wanajaribu kuelekea Ulaya. 

Vyama viwili vya upinaznzai nchini Rwanda vimeuita mpango huo ‘sio halisi’na kuitaka serikali kutatua matatizo ya dnai ya nchi hiyo na sio kubeba msalaba wan chi tajiri 



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/phKrkym
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI