Mwinyi Amfunda Polepole Alipokwenda Kuaga Kuelekea Malawi Kuanza Kazi



RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amemueleza Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole umuhimu wa kwenda kuifanyia kazi na kuipa kipaumbele Sera ya Diplomasia ya Uchumi nchini humo.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo alipokutana na Balozi Polepole Ikulu ambaye alikwenda kuaga tayari kuelekea katika kituo chake kipya cha kazi nchini Malawi.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi amesema kwa sasa Tanzania imeelekeza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi na nchi za nje ambayo ndio dira ya ushirikiano na nchi nyingine kiuchumi.

Amemsisitiza kiongozi huyo kwenda kuifanyia kazi sera hiyo nchini Malawi hasa katika sekta ya biashara.

“Zanzibar ina mazao mengi yanayotokana na bahari ambayo ni bidhaa muhimu katika biashara nje ya nchi wakiwamo dagaa ambao bado hawajapata soko Malawi,” amesema.


Amesema kwa sasa biashara ya dagaa zinazotoka Zanzibar zinafanyika zaidi katika nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).

Pia amemweleza kuwa Tanzania ilishiriki vyema katika kupigania uhuru wa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika ikiwamo Malawi na kutaka akaendeleze uhusiano na ushirikiano wa kimipaka ili kukinga vitendo viovu.

Rais Mwinyi amempongeza Balozi Polepole kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo na kumhakikishia kwamba serikali yake itampa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza jukumu hilo.


Balozi Polepole amemuhakikishia Rais Mwinyi kwamba atayafanyia kazi maelekezo yote aliyompa kwa kutambua kwamba Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kuwa kwa vile Zanzibar hivi sasa imejikita kuweka mikakati yake katika kuimarisha uchumi wa buluu atahakikisha sera hiyo anaifanyia kazi kwa kutafuta fursa hasa zile za biashara zinazotokana na rasilimali za bahari ikiwamo dagaa.

Pia amempongeza Rais Mwinyi kwa kuendeleza na kuukuza uchumi wa Zanzibar hasa katika mikakati yake ya sera ya uchumi wa buluu ambayo aliahidi kwa upande wake kwenda kuifanyia kazi.

Balozi huyo pia amekutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud ofisini kwake na alimweleza kuwa Tanzania inaweza kujifunza katika maeneo meingi yakiwamo ya kilimo na biashara kutoka Malawi na kuibua vyanzo vipya vya kibiashara.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/ZB0iVye
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI