Nimemsomesha, Nimegharamika, Leo Kaniacha Anaolewa na Mtu Mwingine

Wakuu nilikutana na huyu binti miaka kadhaa iliyopita mimi nikiwa nimepangiwa kazi mkoa fulani katika mihangaiko yangu nikakutana na huyu binti nilitokea kumpenda, mzuri kisura na kitabia very innocent niliamini kwake nimefika baada ya kash kash nilizopitia katika mahusiano ya nyuma.

Wanasema usiusemee moyo ila najua yule binti alinipenda kidhati tena moyoni kabisa na mimi kwangu she was a queen na niliapa kumuoa baada ya yeye kumaliza masomo yake. Binti huyu kwao ni familia maskini nikisema familia maskini ni familia maskini kisawasawa. Baba yake alifariki miaka kadhaa nyuma kabla sijaonana nae hivyo aliishi na mama yake na wadogo zake ni story ndefu kuhusu familia yao. Mimi nikawa ndio kama msaada katika familia yao, sikua na hiyana na nilisaidia niwezavyo kwani binti yule nilimpenda kutoka moyoni.

Yule binti alimaliza shule na kuhitajika kwenda chuo lakini familia ikawa haina uwezo wa kumsomesha na mkopo alikosa. Akakosa raha na ikawa kama jukumu ni langu. Mama yake aliniita tushauriane kwasababu kwao nilikua nafahamika. Kwakuwa mimi nilisema nitamuoa binti wakashauri nimsomeshe kama nina nia yakweli. Uwezo wa kumsomesha nilikua nao nikakubaliana na tukaandikishana kwamba namsomesha mimi lakini mwisho wa siku yeye atakuja kuwa mke wangu na hata mahari sintolipa kwani itakua imeingia huko.

Familia ilinishukuru sana kwani waliamini kusoma kwa binti itakua afadhali katika ukombozi wa maisha yao. Binti alikuwepo wakati maandikishano yanafanyika na mashahidi walikuwepo nakumbuka binti alilia yule akiapa kunipenda milele na mapenzi tuliyofanya siku hiyo siwezi kusahau ilikua best sex ever.

Wakuu nifupishe binti alianza chuo kila kitu nililipa nauli hosteli ada matumizi kila kitu ilikua mimi,mwaka wa kwanza ukaisha vizuri mapenzi yanachanua.Likizo naenda likizo zao anakuja, mama mtu alinishukuru sana. Mwaka. Mwaka wa pili matatizo yakaanza nikipiga simu naambiwa yuko library mara assignment nikiuliza zaidi anakua mkali nikasema labda labda kweli shule lakini hata mimi nilisoma muda wa kuongea na mwenzi wangu nilikua nao nikasema labda shule ya sasa ni ngumu. Binti akabadilika majibu ya jeuri nikaenda kuongea na mama yake amkanye naona akajirekebishe na kweli akatulia maisha yakaendelea. Upside zikiwa chache. Mahusiano yalitawaliwa na migororo

Kufupisha Miezi kadhaa imepita binti kaniandikia meseji eti "NAKUSHAURI UTAFUTE MWANAMKE MWINGINE MIMI SIKO TAYARI KUWA NA WEWE NIKUTAKIE MAISHA MEMA"

Naandika huu uzi wakuu acha nikipiga simu haipokelewi mara haipatikani. Nikampigia mama yake kumuuliza kama anajua lolote akasema hafahamu. Nikaomba likizo kazini nifatilie sikuamini siku naambiwa ana mimba na anaishi na mwanaume mwingine. Nilitamani ardhi ipasuke kumbe ndio maana niliandikiwa ule ujumbe nikajiuliza maswali bila majibu,basi angefanya nisijue na mimba juu kapata inauma sana. Kumuuliza mama yake hana analonijibu, kumbe chuo kapostpone sijui anaishi na huyo mwanaume moja ya mitaa Dar, yote hiyo nafatilia kwa baadhi ya marafiki zake na kibaya zaidi huyo mwanaume alishamlipa tena huyo mama pesa nyingine. Na ndio kamchukua binti yake.

Nimechukia kuuziwa mbuzi kwa gunia.Love is blind inakuwaje sikuona yote hayo? Why me..Why.. Najiuliza sipati majibu, sikuwahi kupenda kama nilivyompenda huyo binti. Nilimpenda kutoka moyoni na kujitoa kwake sijawahi kumfanyia mwanamke yoyote niliyomfanyia leo ameniacha kwenye mataa na nyodo juu, kuna muda natamani ningekuwa na bastola nimsambaratishe ila that is not me. Juzi nimeona whatsup kaweka picha yake tumbo kule na namba yake nikafuta.

NILICHOFANYA;

Nimepeleka hii kesi Mahakamani kwasababu tuliandikishana kama mke nimekosa basi nilipwe gharama zangu najua haiwezi kuziba pengo kufuta maumivu naona is the least i can do for my self. Wakuu nifanyaje au nimekosea kupeleka shtaka polisi tumeshaitwa mara mbili hakuna mtu aliyetokea upande wao. Nimetokea kuwachukia wanawake sana. Kwanini mnatufanyia hivi jamani tuwapende vipi. Nimekaa hapa kitandani nimewaza mawazo mengi moyo wangu kama barafu naishia kusononeka.

Sijui nimfanyie kisasi gani aumie kama mimi nilivyoumia.

from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/xChdJlb
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI