Pablo: Simba Tulieni, Tunawapiga Yanga Jumamosi Uwanja wa Mkapa





WAKATI Simba SC wakitua Dar wakitokea Afrika Kusini, kocha mkuu wa kikosi hicho, Pablo Franco, akilini mwake alikuwa akiiwaza Yanga kuelekea mchezo wa Jumamosi hii, huku akiwaambia mashabiki wa Simba watulie, ushindi upo.

 

Pablo ambaye hii itakuwa ni mara ya pili kukutana na Yanga tangu atue Simba baada ya awali kutoka 0-0, ameweka wazi kuwa, wanaelekeza nguvu zao katika mchezo huo kwa lengo la kupunguza pengo la pointi na wapinzani wao hao, hivyo lazima washinde.

 

Pablo ametoa kauli hiyo kufuatia Simba juzi Jumapili kuondolewa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

 

Simba inatarajia kucheza na Yanga Aprili 30, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar. Yanga wanaongoza ligi kwa pointi 54, wakati Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 41.



Akizungumza na Spoti Xtra, Pablo alisema nguvu na mapambano kwa sasa wanaelekeza katika mechi zao za ligi kuu, ikiwemo mchezo ujao dhidi ya Yanga.

 

“Katika michuano ya kimataifa, safari yetu imefikia mwisho, tumeondolewa jambo ambalo halikwepeki japokuwa wachezaji wamepambana kutafuta matokeo mazuri, lakini haikuwa upande wetu.

 

“Tunachokiangalia ni kuongeza nguvu zaidi katika mechi zetu zilizobaki kwenye ligi, tunaelewa hakutokuwa na mechi nyepesi kwetu ukianzia ambayo inakuja mbele yetu dhidi ya Yanga, lazima tushinde.

 

“Tunachokiangalia ni kuona timu inapata matokeo mazuri ambayo ndiyo jambo muhimu ili kupunguza pengo kubwa la pointi kati yetu.”

Simba imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo kuanzia msimu wa 2017/18.

STORI NA IBRAHIM MUSSA/GPL


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/4689Tsd
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI