Rais Samia asema anazielewa sababu Chadema kususia



Rais Samia Suluhu Hassan
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema anaelewa sababu ya chama kimoja ambacho hajakitaja, kimekataa kushiriki mchakato wa majadiliano ya kutafuata muafaka mazingira ya ufanyaji siasa na kuleta umoja wa kitaifa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Samia ameyasema hayo jioni ya Jumamosi tarehe 23 Aprili, 2022 wakati akizungumza na Watanzania waishio Marekani (Diaspora), Washington DC na kueleza kuwa bado anaendelea na majadiliano nao ili wajiunge na wenzao.

“Tumeanza mazungumzo na vyama vya siasa kupitia baraza lao la siasa tumefamnya mkutano wa awali na kuunda kikosi kazi chao wenyewe watajadili mambo ambayo wenyewe wamepanga watatuletea.

“Kuna chama cha siasa kimoja bado hakijakubali, bado naendelea na mazungumzo nao na naelewa kwanini hawajakubali moja kwa moja kujiunga bado naendelea na mazungumzo nao tunakwenda vizuri na namatumaini watajiunga na wenzao,” amesema Rais Samia.


 

Rais Samia ambaye alipokewa na mabango na baadhi ya Watanzania waliokuwa wakipeleka ujumbe wa kutaka mchakato wa Katiba mpya amesema, “hali ya kiisasa tupo viruri mambo yote wanazungumza kikosi kazi watatuletea.”

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ndicho amabcho hakikushiriki mikutano na makongamano yote yalioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania n ahata yale ya Baraza la Vyama Vya Siasa.

Chadema wamekuwa na msimamo huo kwa kile wanachodai kuwa mchakato huo hauna nia ya dhati ya kupatikana kwa Katiba Mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.


Chama hicho kikuu cha upinzani mara baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kilitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi wowote nchini hadi pale Katiba Mpya itakapopatikana.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/mtvodkp
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story