Shaffih Dauda "Simba wanaweza kuiangalia TP Mazembe kama timu ya mfano kwao"


Kushinda ubingwa wa Afrika au kuwa na matokeo mazuri mfululizo kwenye mashindano ya CAF Champions League au Confederation Cup ni jambo linalohitaji muda.

Simba wanaweza kuiangalia TP Mazembe kama timu ya mfano kwao, vilevile naamini hata Mo role model wake ni Moise Katumbi kwa namna ambavyo aliichukua Mazembe na kuifikisha hatua ya kushinda mataji ya Afrika.

Katumbi aliichukua TP Mazembe mwaka 1997 lakini mwaka 1998, 1999 na 2000 Mazembe haikushiriki kabisa mashindano ya CAF. Mwaka 2001 Mazembe ilishiriki CAF Champions League kwa mara ya kwanza tangu Katumbi amekuwa Rais wa klabu! Wakifika hadi Makundi na kushika mkia kwenye Kundi A.

Mwaka 2002 Mazembe ilimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi ndio mafanikio ya kwanza baada ya uwekezaji wa miaka mitano. Mwaka 2004 wakatolewa mapema na Zamalek, 2005 wakatolewa tena hatua ya awali, 2006 hawakushiriki kabisa! Mwaka 2007 waliishia raundi ya pili wakatolewa na Rabat.

Mwaka 2008 wakafika hadi hatua ya makundi na kumaliza katika nafasi ya tatu, 2009 wakafanikiwa kutwaa ubingwa, 2010 wakachukua tena ubingwa, 2011 walikuwa disqualified baada ya kumtumia mchezaji ambaye haruhusiwi kwa mujibu wa kanuni. Kwa hiyo unatakiwa kupata picha 1997 Moise Katumbi ndio aliichukua Mazembe akafanikiwa kuingia fainali mwaka 2009 (miaka 12 baadaye) baada ya kuingia fainali ikawa ni desturi ya Mazembe kuchukua ubingwa au kufika hatua za juu kwa sababu hawakubahatisha kufika huko.

Simba inafika Robo Fainali mara tatu ndani ya misimu minne haimaanishi wanastahili kwenda Nusu Fainali au Fainali.

Kwa mfano Simba wangeweza kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Orlando kwa mikwaju ya penati, vipi kuhusu misimu miwili au mitatu ijayo wanaweza kuwa na mwendelezo wa kufika huko? Ishu sio kuingia nusu Fainali au Fainali, unaweza kutumia nguvu nyingi ukafanikiwa kuingia, je litakuwa eneo lako la kudumu? Kwangu naona bado Simba ipo kwenye njia sahihi, jambo muhimu ni kuendelea kutengeneza mifumo na kuamini kwenye sehemu ambayo wapo sasa hivi na kutokuwa na haraka au kutaka kuendesha timu kwa presha zinazotoka nje.

Ubingwa wa CAF Champions League na Confederation Cup sio jambo la kulala na kuamka IT’S A PROCESS


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/EPt0lXD
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story