Simanzi; Miili Ya Wanakwaya Waliokufa Ajalini Njombe Yaagwa
SIMANZI na majonzi! Miili tisa ya waumini wa Kanisa Katoliki mkoani Njombe waliofariki kwa ajali ya gari iliyotokea Kijiji cha Igima wilayani Wanging’ombe Aprili 24, 2022 imeagwa katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki la Njombe.
Akizungumza wakati wa ibada ya kuaga miili hiyo leo Jumanne Aprili 26, 2022, Mkuu wa Mawasiliano wa Jimbo hilo, Padri Eusebius Kyando amesema Umoja wa Vijana Katoliki Jimbo la Njombe (Uvikanjo) pamoja na walezi wao walipata ajali wakiwa wanarudi katika safari yao ya kitume walikokwenda kuwatembelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Dorothea Upendo kilichopo Ibumila Parokia ya Mtwango.
Amesema katika ajali hiyo, watu watatu walifariki papo hapo na wengine sita walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu hospitalini.
Amesema toka mwaka 2020 Uvikanjo Parokia ya Njombe wamekuwa wakifanya kazi ya utume kwa kutembelea jumuiya ndogondogo na watu wenye mazingira magumu na kufanya matendo ya huruma katika vituo hivyo.
“Vijana wetu walipata ajali na wengine kufariki wakiwa katika harakati za kitume yaani kueneza injili kwa njia ya matendo mema” amesema Padri Kyando.
Amesema utume huo umewafanya vijana wengi kuimarika katika imani na hofu ya Mungu hasa katika kumpenda Mungu kupitia wahitaji.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/76v3aMX
via IFTTT
Comments
Post a Comment