Wanaume Waongoza Vifo Vitokanavyo na Ukimwi



Dar es Salaam. Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (ATF) umesema vifo vitokanavyo na Ukimwi vimekua vikiongezeka miongoni mwa wanaume wenye maambukizi, huku tabia hatarishi zikitajwa chanzo.

Hata hivyo, vifo hivyo vimetajwa kuendelea kupungua miongoni mwa wanawake waliopata maambukizi hayo.

Hayo yamesemwa leo Aprili 25, 2022 na Meneja wa Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (ATF) Peter Kivugo alipokuwa akitoa mafunzo kwa waandishi na maofisa masoko wa vyombo vya habari juu ya dhana ya serikali ya uanzishwaji wa mfuko huo.

“Vifo vinavyotokana na magonjwa nyemelezi kwa wanawake vimepungua lakini kwa wanaume vinapanda, wengi wanakufa mapema kutokana na kushindwa kuzingatia maelekezo ya dawa na kujizuia katika tabia hatarishi ambazo zinawasababisha kupata maambukizi mapya na magonjwa mengine ya zinaa,” amesema Kivugo.

Kivugo ametaja takwimu za vifo vitokanavyo na Ukimwi kwa mwaka 2019 watu wazima miaka 15 na zaidi vilikuwa 21,529 ambapo wanaume walikuwa 12,225 na wanawake 9,304 huku watoto chini ya miaka 15 vilikuwa 5,900 na kufanya jumla ya vifo 27,429.

Akizungumzia mfuko huo Mkurugenzi wa uraghabishi Tacaids, Jumanne Isango alisema Serikali ilianzisha ATF mwaka 2015 kwa lengo la kuwa na mfuko ambao utatusaidia kukusanya rasilimali za ndani.

“Mfuko umekua ukichangia maeneo mengi ya kupambana na ukimwi huu mfuko una umuhimu mkubwa kwani lengo ni kujitegemea,” alisema.

Mwananchi



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Xi5A87b
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI