Azam FC chalii, Coastal Union yaifuata Young Africans

 


Mkwaju uliopigwa na Mubaraq Hamza umeipeleka Coastal Union hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ya Tanga, wakiitoa Azam FC.


Mchezo huo wa pili wa Nusu Fainali ya ‘ASFC’ ulishuhudia hali ya furaha kwa Coastal Union ikitamalaki katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


Dakika 120 za mchezo huo zilishuhudia timu hizo zikishindwa kufungana huku zikishambuliana kwa zamu, lakini Coastal Union walifika mara nyingi zaidi langoni mwa Azam FC.


Katika mikwaju ya Penati Coastal union ilipata mikwaju 6 dhidi ya 5 ya Azam FC ambayo ilipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.


Ushindi huo wa Coastal Union unaipeleka mbele ya Young Africans iliyotangulia Fainali jana Jumamosi (Mei 28), kwa kuifunga Simba SC jijini Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba.


Mchezo wa Fainali utapigwa Julai 02 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao leo Jumapili (Mei 29) umetumika kwa mchezo wa Nusu Fainali.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/O0YoexJ
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI