Real Madrid washinda taji la 14 la Ligi ya Mabingwa
Bao moja la Vinicius Junior kunako dakika ya 59 lilitosha kuihakikishia Real ushindi wa 14 wa kombe la Ulaya mbele ya mashabiki 80,000 mjini Paris.
Real Madrid kwa mara nyingine inarejea nyumbani na kombe, Madrid imetumia fursa na kuwaacha wengi wakijiuliza ni kwa jisi gani wameambulia ushindi wa konbe hilo.
Jaribio la mshambuliaji Karim Benzema liliamuliwa kwa utata kuwa ameotea.
Mchezaji wa Liverpool Mohamed Salah akinyimwa nafasi ya kuikomboa mara tatu timu yake na mlinsa lango wa Real Madrid Thibaut Courtois.
Usalama uwanjani
Fainali hio ilicheleweshwa kwa zaidi ya dakika 35 kwa sababu za usalama.
Shirikisho la Kandanda Barani Ulaya UEFA ililaumu kuchelewa kuwasili kwa mashabiki, lakini mashabiki walilaumu mamlaka kwa kuchelewa kufungua uwanja wa Stade de France.
Mamia ya mashabiki wa Liverpool walimiminika kujaza viti katika uwanja wa Stade de France, polisi wa Ufaransa walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi ili kuwazuia.
"Tumesikitishwa sana na maswala ya kuingia uwanjani na uharibifu wa eneo la usalama ambalo mashabiki wa Liverpool walikabiliana nao jioni ya leo huko Stade de France," ilisoma taarifa iliyotolewa na Liverpool katika kipindi cha pili.
"Hii ni mechi kubwa zaidi katika soka la Ulaya na wafuasi hawapaswi kuwa na matukio ambayo tumeshuhudia usiku wa leo. Tumeomba uchunguzi rasmi kuhusu sababu za masuala haya yasiyokubalika."
Ngoma itambae
Mlinda lango wa Madrid Courtois alikuwa muhimu, na kuokoa kombora kutoka kwa Mo Salah na kumfanya mchezaji bora wa mechi. Lakini kwa uzoefu, na mfululizo wa kujimbanua ilikuwa uchawi tosha kwa timu ya Real Madrid.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/gh18xKO
via IFTTT
Comments
Post a Comment