Tuhuma za Gambo Ngoma Nzito, Wanane Wahojiwa

 


Tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zilizoibuliwa wiki iliyopita Jijini Arusha na kusababisha watumishi sita kusimamishwa kazi, zinazidi kulitikisa Jiji hilo baada ya idadi ya wanaohusishwa nazo kufikia wanane.

Wiki iliyopita Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwasimamisha kazi watumishi hao wa Halmashauri ya Jiji la Arusha akiwamo Mkurugenzi wake Dk John Pima kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na kulikabidhi suala hilo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili ichunguze.

Katika sakata hilo, Mbunge wa Arusha mjini (CCM), Mrisho Gambo alimtaja Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa, Kenan Kihongosi kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Hata hivyo, jana Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, James Ruge aliliambia gazeti hili kuwa idadi ya wanaohojiwa na taasisi hiyo imeongezeka kutoka sita wa awali hadi nane kutokana na kubaini kuwepo kwenye mnyororo wa tuhuma hizo.

“Ukiachilia mbali wale watuhumiwa sita tuliokabidhiwa, lakini sasa tumeongeza wengine wawili ambao katika uchunguzi wetu tumeona tuwahoji hivyo watuhumiwa wamefikia wanane lakini wengine wengi watafuata,”alisema Ruge.

Hata hivyo Kamanda Ruge hakuwa tayari kuwataja watuhumiwa hao kwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi ambao wamebaini kuwepo kwa mnyororo mrefu lakini kwa kuwa kazi hiyo wanaifaya kwa kushirikiana na taasisi nyingi ikiwemo benki.

Vita vya Gambo na kigogo wa UVCCM bado moto

“Maneno ni mengi huko mtaani lakini hatuwezi kujibu na kuharibu kazi yetu, kubwa ambayo tumeifanya, hivyo niwaombe wananchi kuwa watulivu tukamilishe kazi yetu na tutatoa taarifa iliyokamilika,”alisisitiza kamanda huyo

Sakata lilivyoibuka

Mei 24, 2022, Waziri Mkuu akiwa ziarani mkoani Arusha, aliwasimamisha kazi maofisa sita wa Jiji la Arusha akiwemo Mkurugenzi wake Dk John Pima kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za Jiji na tuhuma za kughushi nyaraka.

Wengine waliosimamishwa kazi ni Mweka Hazina wa Jiji,Mariam Mshana, Innocent Maduhu (Mchumi), Alex Tlehama na Nuru Saqwar kutoka Ofisi ya Mchumi na Joel Mtango ambaye ni Afisa Manunuzi wa zamani wa Jiji hilo

Akizungumza wakati akitoa maagizo hayo, Waziri Mkuu alisema amefikia uamuzi huo kwa kuwa hawezi kuvumilia kuona fedha za umma zikitumika kinyume na taratibu ambapo alimtaka CAG naye kuanza uchunguzi

Alimtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutafuta nyaraka zote kubaini undani wa ubadhirifu huo huku akimtakaKamanda wa Takukuru wa Mkoa kufuatilia kwa ukaribu wahusika wote.


Siku hiyo Gambo ni kama alikoleza moto pale alipomtuhumu Kihongosi kuwa kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Jiji la Arusha katika matumizi mabaya ya fedha na kudai Kihongosi kupitia akaunti ya mkewe aliingiziwa Sh2 milioni.

Hata hivyo Kihongosi ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) na Kamati kuu ya CCM na amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha alipoulizwa alisema kamati ya maadili ya CCM ndio yenye uhalali kuchunguza tuhuma dhidi yake .



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Z1pN26X
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI