Collabo ya Diamond Platnumz na Ney wa Mitego Haitawahi Tokea Tena

 


Kuna 'kolabo' nyingi. Lakini ya Ney na Mondi ya "Muziki", inabaki kuwa bora kwa miaka 10 hii. Undava wa Ney na 'ulaini' wa Mondi. Umezalisha kitu tofauti chenye sanaa kubwa. Ney akiigiza nunda, Mondi akicheza 'sini' inayofanya Ney aonekane hana facts.


NEY

Muziki wenu ushirikina, ndo umetawala, Q-Chillah analalama, anasema umemroga, Mganga wako aliyekutoa, umemkimbia hujamlipa, Bila skendo za magazeti, basi husikiki...

DIAMOND

Ah, mi ni mti wenye matunda, milele siogopi kupigwa mawe, Ubaya wenu wengi "kayumba", elimu mlitupa sadakalawe...


Ney na porojo za ushirikina kwenye 'gemu'. Zinajibiwa kikatili, kwa lugha laini na sauti 'bembelevu'. Ni kama Mondi kamchoresha Ney kuwa hayo ni mawazo ya waliokimbia umande. Kwamba ukosefu wa elimu hufanya watu waamini mafanikio huletwa na uchawi.


NEY

Bado hujanishawishi, Bongo Fleva inanipa kichefuchefu, Kwanza nyie malimbukeni wa umarufu, Mnaleta maringo mpaka kwa mashabiki, Wabana pua nyie watoto sio ridhiki, Mnavaa nguo za dada zenu, zinawabana mapaja, Nyie makakaduu..

DIAMOND

Hata mimi nina mengi ninayajua, ila we mtemi utaanzisha utata, Michezo yenu kutoboa pua, bora ninyamaze usinipige mbata...


Chid Benzi, baada ya kutoboa pua ilileta gumzo sana. Aina ya muziki wake kilikuwa kitu tofauti sana na alichofanya. Ney anaponda 'watoto' wanavaa nguo za dada zao, huku 'kaka yao' akiwa katoboa pua? Hili dude ubunifu ni 100%. Mistari na midondoko mitamu. Amazing sana!


Cc @blessed_tillah



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/gysR0tW
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI