Kesi ya kina Mdee kusikilizwa siku 14 mfululizo




HATIMA ya endapo Halima Mdee na wenzake 18 wataendelea kusalia kuwa wabunge itajulikana ndani ya siku 14 za usikilizaji wa shauri namba 27 la mwaka 2022. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Shauri hilo linalosikilizwa na Jaji Mustapha Ismail katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam limefunguliwa na Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya Bodi ya wadhamini ya Chadema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Halima na wenzake wanapinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho mara baada ya Baraza Kuu la chama hicho kubariki uamuzi wa Kamati Kuu ya kuwafukuza uanachama kwa makosa ya usaliti.

Leo Alhamisi tarehe 29 Juni, 2022, Mahakama hiyo imetoa kibali kwa wajibu maombi wote kuwasilisha viapo kinzani kesho Alhamisi tarehe 30 Juni, 2022 tayari kwa kuanza kusikiliza shauri hilo.


 

Hatua hiyo imejiri baada ya Kibatala kuiomba Mahakama hiyo kuondosha mapingamizi waliyowasilisha awali ili kupisha usikilizwaji wa shauri hilo kwa kuwa limefunguliwa mahakamani hapo kwa Hati ya dharura.

Jaji Mustapha Ismail amekubali ombi hilo na kuamua kuondoa mapingamizi hayo kabla ya shauri la msingi kuendelea kusikilizwa ambapo amesema kuwa amri ya zuio itaendelea mpaka shauri la msingi litakapofika mwisho.

“Baada ya kusikiliza hoja za Mawakili nimeamua Hati ya mapingamizi ya awali inaondolewa mapingamizi yote hayatataendelea”


Pia Jaji Mustapha amesema kuwa amri ya itaendelea mpaka mwisho wa shauri la msingi.


 

Juma Magoma
9h
1

Jambo kubwa hapa ni ukikwaji was katiba ya nchi jambo ambalo ni aibu kubwa, kwani hawa wabunge wana maslahi gani ya taifa hadi tushinikize aibu ya kuvunja kanuni tulizojiwekea, kwamba mbunge atakoma ubunge pale atakapo kosa sifa ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa anachokiwakilisha. Jamani mnatupa taabu kuona hili hadi sisi mambumbumbu tunashindwa kulivumilia. Mbona mna cheza na katiba?.. Hawa kama ni watu bora basi wangepewa kazi nyingine kama vile ukuu wa mkoa, wilaya, ubalozi nk. Hatuelewi kabisaaa maana sio mwanzo watu kufukuzwa uanachama na kukosa sifa hata kwa upande wa chama tawala. na pia jambo kama lipo mahakamani iweje wanaendelea na nyadhifa ambazo kimsingi zimelalamikiwa? Busara itumike tuepuka ubabe.!!!Zaidi

Jibu

GUEST_EZe9pNxyD
10h
1

kumbukeni shauri linaloskilizwa na ombi la kuomba kulishtaki baraza la wadhamini la chadema na mwana sheria mkuu wa tanzania kupinga kufukuzwa kwao unachama,mahakama kuu ilikubali ombi hilo ndiyo wanafungua shtaka hilo rasmi. Wakikataliwa bado watakuwa na haki ya kukata rufaa, hivyo safari bado ni ndefu. Na spika hawakumbatii anafuata taratibu za sheria maana hawa wabunge waliapishwa sasa suala kwamba walifoji ni mahakama ittyolea uamuzi na siyo wanachadema kuweni wapòle msikilize sheria.Zaidi



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/kDG9gbl
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI