Mwigulu Nchemba "Hatuwezi Kuacha Kukopa Kuogopa Deni Kuwa Kubwa"

 


Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema haiwezekani kuacha kukopa kwa kuogopa deni kuwa kubwa, mikopo ya Serikali ni kwa ajili ya Maendeleo ya Miradi mikubwa ya Nchi na siyo ya kulipia Mishahara au Matumizi ya kawaida


Amesema Deni la Serikali kwa sasa uwiano wake na Pato la Taifa ni 31% wakati ukomo ni 55%, Deni la Nje kwa Uwiano wa Pato la Taifa ni 18% wakati ukomo wake ni 40%, Deni la Nje kwa mauziano ya nje ni 142% ukomo ni 180%


Waziri ameongeza "Tunafurahia 4G na 5G lakini Mkongo wetu wa Taifa ni deni, miradi ya aina hiyo ni mingi. Mradi ukishakopewa hauwezi kusimama, fedha zinapoingia ndivyo deni linavyokua. Mfano kuna madeni nimesaini yalipwe ambayo yalikopwa kabla sijazaliwa"




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/UV56W38
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI