Somo la Historia ya Tanzania Kuanza Mwakani



Somo la Historia ya Tanzania kama somo linalojitegemea litaanza kufundishwa katika shule za msingi na sekondari Januari mwakani.

Maandalizi ya somo hilo kuanza kufundishwa kama somo linalojitegemea yamekamilika kama alivyoagiza Rais wa awamu ya tano, John Magufuli kwamba lianze kufundishwa kama somo linalojitegemea.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chumbuni, Ussi Salum Pondeza (CCM). Pondeza alitaka kujua ni lini somo hilo la historia litaanza kufundishwa kama Rais John Magufuli alivyoagiza lianze kufundishwa kama somo linalojitegemea shuleni.

Kuhusu swali la nyongeza la lini mitaala ya elimu iliyoboreshwa itaanza kutumika kufundishia, Kipanga alisema mitaala hiyo mipya imekamilika na itaanza kutumika Januari mwakani. Kipanga alisema kinachofanyika sasa ni kufanya maandalizi ya vifaa vinavyotakiwa kutumika katika kufundisha kwa kutumia mitaala hiyo mipya ya elimu.

Pondeza pia alitaka kujua wataalamu kutoka Zanzibar wameshirikishwaje katika kuandaa mtaala wa somo la historia ili kuandikwa kwa usahihi ikizingatiwa kuwa historia ya Zanzibar na Tanzania Bara ipo tofauti.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/QEyJqvp
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI