AIBU: Bondia Mandoga Mtu Kazi Apingwa Tena KTO Afunguka "Hii ni Kama Ajali"


Bondia mwenye tambo na maneno mengi kutoka Mkoani Morogoro, Karim Mandonga kwa mara nyingine amechezea kichapo katika pambano la "Usiku wa Kisasi" dhidi ya Shabani Kaoneka pambano lililopigwa usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Majimaji Songea.


Pambano hilo la Mandonga ambalo lilikuwa pambano la utangulizi lilijipatia umaarufu mkubwa na kusubiriwa kwa hamu na wapenzi wafuatiliaji, limewastaajabisha watu wengi kutokana na matokeo yake kwani Mandonga alipigwa kwa TKO katika raundi ya nne dhidi ya Shabani Kaoneka.


Akizungumza baada ya Pambano mandonga alisema; "Hii ni kama ajali kazini, mtu anayependa kazi na asiyependa ajali inamkuta, lakini simuhofii Shaban Kaoneka, naweza sema pia ni mipango ya Mungu amepanga nipoteze na mimi sina uwezo wa kumbishia Mungu."- Mandonga aliiambia Azam TV.


Itakumbukwa, Mandonga amejipatia umaarufu mkubwa nchini licha ya kupoteza mapambano yake mawili mfululizo yaliyopita kutokana na kujiamini pamoja na tambo zake anazozionesha kabla ya mapambano yake.


Neno moja kwa Mandonga MTU kazi



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/nu59MKX
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI